Blogroll

Jumamosi





Tupo kwenye ukumbi AICC arusha kwenye kongamano la vyombo vya habari. Ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari

 

Posted on 00:23 by Unknown

No comments



DSC_0053
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.

“Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.

Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.

“Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.

Posted on 00:20 by Unknown

No comments










Magari yaliyozama baada ya ardhi kumezwa na maji

 Wakati mvua kubwa zimenyesha Dar es salaam siku kadhaa zilizopita baadhi ya watu waliilalamikia Serikali kwamba imefanya uzembe manake kama ingekua imejenga miundombinu vizuri, maeneo ambayo yangekumbwa na maafuriko ni machache.
Post hii ni maalum kwa ajili ya hiki kilichotokea kwenye jiji la Baltimore Marekani ambapo mvua kubwa imesabisha kuzama kwa mtaa uliokua umejengwa vizuri kabisa lakini umemezwa na magari yaliyokua yamepaki juu yake.

 Screen Shot 2014-05-02 at 11.03.44 PM
Screen Shot 2014-05-02 at 11.04.01 PM

Posted on 00:14 by Unknown

No comments

http://4.bp.blogspot.com/-rup9GsnMX8U/U2HUdSljY_I/AAAAAAAARJQ/_LLk6yGItkM/s1600/02.jpg
Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwaasa wabunge wote kushiriki kikamilifu katika kamati zao kizalendo kwa kujali nchi yao ili ipatikane bajeti yenye tija kwa taifa leo (jana) wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.

http://2.bp.blogspot.com/-OtOFpq8RUKo/U2HUaITF4gI/AAAAAAAARJE/NyW2gFgsWlM/s1600/03.jpg 
Waziri wa Fedha Saada Mkuya  Salum akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya Serikali kwa wabunge leo (jana) jijini Dar es salaam inayotarajia kuanza kutumika kwa mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015.

http://3.bp.blogspot.com/-obOedfMxDaw/U2HUaSkfxvI/AAAAAAAARJA/KpjYbkiIICQ/s1600/04.jpgWaziri Mkuu wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda  akizungumza na wabunge wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam. 

Posted on 00:11 by Unknown

No comments

Ijumaa


Screen Shot 2014-05-02 at 1.26.42 PM
 Ni rasmi kwamba Clouds Media International imepewa leseni ya kurusha matangazo katika nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE) ambapo mkurugenzi Mtendaji Joseph Kusaga amesema sasa kituo cha Clouds TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa mataifa mbalimbali.
Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni maarufu sana kwa vijana nchini Tanzania, hata hivyo sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo kwenye Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa vipindi kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa.
Akieleza zaidi Kusaga amesema “Leo ni siku ya kihistoria na alama ya hatua moja katika mpango wetu wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa kupitia matangazo kwa njia ya mitandao’’.

Screen Shot 2014-05-02 at 1.27.41 PM

Clouds TV kimataifa haitotoa tu burudani lakini pia itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja wa nchi za falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina yao.
Vituo vya televisheni katika Umoja wa falme za kiarabu vipo vingi na vyenye ushindani mkubwa, lakini Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi ya kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika chaneli yenye uwezo wa kuwahudumia zaidi ya watazamaji takribani milioni 3.5 kutoka katika nchi za Afrika. Kwa sasa hakuna kituo kinachotoa huduma hii na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.
Clouds TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani, tamthilia, maigizo, ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za mashariki, magharibi na kusini mwa bara la afrika na itapatikana kwa watazamaji walio katika Umoja wa falme za kiarabu kupitia huduma ya IPTV inayotolewa na Etisalat na Du.
Clouds TV kimataifa itarushwa kupitia mamlaka ya Abu Dhabi ijulikanayo kama twofour54, ikiungana na vituo kama FOX na CNN.
Clouds TV kimataifa itaanza kurusha matangazo ya majaribio katika wiki chache zijazo kabla ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.

Posted on 07:36 by Unknown

No comments


Screen Shot 2014-04-30 at 2.08.18 AM
Mpaka sasa video hii imetazamwa zaidi ya mara laki moja na elfu 30 kwenye mtandao wa Youtube toka ianze kuonyeshwa April 29 2014 ikiwa ni video ya kipekee na ya kiwango kingine cha juu tofauti na ilivyozoeleka kwa Sauti Sol.
Mtandao wa Kenya ghafla.co.ke umeripoti kwamba imefahamika video hii imezuiwa kuchezwa kwenye TV stations mbalimbali za Kenya kwa sababu imevunja maadili.
Kwenye Mdundo Awards jana usiku Bien Aime wa Sauti Sol alisema mwanasheria wao anashughulikia ishu ya kufungiwa kwa video yao ambayo imeambiwa inachochea ngono kutokana na uwazi wa wanaookenana ndani yake.
Hii itakua video nyingine iliyochukua headlines zinazofanana na ile ya P Unit ‘you guy’ ambayo ilifungiwa na CITIZEN TV kwa sababu ya mrembo alieliachia umbo lake kwa sana.

Posted on 07:34 by Unknown

No comments



mlipuko
Usiku wa kuamkia leo Maafisa nchini Nigeria wametoa taarifa kuhusu mlipuko uliotokea na kuua watu 19 katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini 6 kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani pia magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya ambao uko karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.
 nyanya
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa,Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari,Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa.
Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja,Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao.

Posted on 07:32 by Unknown

No comments