Blogroll

Alhamisi

Mambo yanaendelea kuiva taratibu tayari kuelekea Brazil from 12 June to 13 July 2014. Hiyo itakuwa mara ya pili kwa Brazil kuandaa Fainali za Kombe la Dunia. Jumla ya nchi 32 zitashiriki. Jumla ya mechi 64 zitachezwa katika majiji 12 ya Brazil. Pia itakuwa ni mara ya kwa "goal-line technology" kuanza kutumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia. Spain watakuwa wanatetea kombe hilo baada ya kufunga Holland 1-0 katika Fainali zilizopita.

Posted on 04:09 by Unknown

No comments


Screen Shot 2014-06-04 at 11.08.57 AM
Huu ni mwaliko wa Jagur kuingia Ikulu kwenye sherehe za siku ya madaraka 2014.

Jaguar ni msanii ambae alishiriki kwa kiasi kikubwa sana kwenye kampeni za kumuwezesha Rais Uhuru Kenyatta kuchukua nafasi ya urais wa taifa la Kenya vilevile Jaguar ndio msanii pekee wa kizazi kipya kuingia Ikulu kiurahisi na mara kwa mara kuliko msanii yeyote yule ambapo hii imetokea kwenye utawala wa Rais huyu kijana.
Ukaribu wao umeanzia mbali na ndio maana President hajamsahau Jaguar kwenye ufalme wake ambapo Jaguar kuingia Ikulu ya Kenya sasa hivi sio ishu ngumu kwake na hata anapotaka kuwasiliana na Rais sio ishu yani.

Screen Shot 2014-06-04 at 11.09.04 AM
Makamu wa Rais William Ruto, Rais Uhuru Kenyatta na Jaguar Ikulu weekend iliyopita.

 Pamoja na nafasi aliyoipata Jaguar kuwa karibu na Rais na Makamu wake kama inavyoonekana kwenye picha, msanii huyu ameahidi kwamba nafasi hii ataitumia kuwaweka vijana wa Kenya sehemu nzuri kwa kuyawasilisha mapendekezo na matatizo yao moja kwa moja kwenye mazungumzo na Rais.
Screen Shot 2014-06-04 at 11.09.12 AM
Rais Uhuru ambae amekua akiendesha mambo kadhaa kiujana zaidi na kuyafanya yawe mepesi kuliko awamu zilizopita, amekua akipokea sifa mbalimbali kutokana na maamuzi yake mengine mfano kutotembea na msafari kila wakati ambapo ili kuepusha gharama lakini pia vilevile usumbufu.
Aliwahi kutembea na gari moja tu Nairobi alafu akasimamishwa na askari wa usalama barabarani ambae baada ya kioo kufunguliwa alishangaa kuona President yuko kwenye hilo gari bila msafara wala kelele za king’ora.


Posted on 23:55 by Unknown

No comments


fedha
Bunge la bajeti linaendelea bungeni mjini Dodoma ambapo sasa ni zamu ya wizara ya fedha na uchumi. Bajeti yake imewasilishwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salum ambapo bajeti yake imepita huku suala la deni la taifa likiendelea kuumiza vichwa vya wabunge wengi kwa kuendelea kukua siku hadi siku.
Suala hilo limeonekana kuwashtua wabunge wengi akiwemo Mheshimiwa Christina Lissu ambaye anasema fedha zinazokopwa na kuongeza deni la taifa zimekuwa hazitumiki katika miradi ya maendeleo.
Picha no 6(2)
Mhe. Lissu anasema “Mheshimiwa spika deni la taifa, tumeangalia hotuba ya kamati ya wizara hii ikieleza kwamba deni la taifa limekua kutoka trilioni 21 hadi 29 ikiwa ni ongezeko la trilioni 8 tu kwa miaka 7, kukopa ni sahihi na nchi yoyote inakopa lakini je fedha tunazokopa zinaenda katika miradi ya maendeleo? Mbona ukuaji huu wa deni hauendani na fedha zinazoelekezwa katika miradi ya maendeleo?.”
“Kwa mwaka huu karibu miradi yote ya maendeleo imepelekewa fedha chini ya asilimia 50, mbona ukuaji wa deni hauendani na fedha zilizoenda kwenye matumizi ya maendeleo? inawezekana tunakopa na tuaambiwa deni ni stahimilivu lakini kama fedha haiendi kupunguza matatizo ya wananchi inakuwa haina maana kukopa.”
Suala la kuchelewesha fedha zinazotengwa kwa ajili ya bajeti ya miradi mbalimbali limeonekana kuwagusa wabunge wengi ambapo Mhe. Asupta Mshana anasema;
“Kumekuwepo na tatizo kubwa la fedha tunazoidhinisha kama bunge kutotolewa kwa wakati na kufanya kazi kama zilivyopangiwa, tatizo ni kwamba tunaandaa bajeti kwa kutabiri bila kuwa na fedha mkononi. Ni vyema tukabadilisha utaratibu wa kuandaa bajeti zetu badala ya kuwa na Cash bajeti tuwe na Capital bajeti”
Pamoja na jitihada za serikali kupitia kukusanya kodi je mikakati ya ukusanyaji kodi inatosha? Mhe. David Kafulila anasema;
“Tufike mahala tuwe na mkakati wa kutosha kuhakikisha maeneo yote ambayo hatukusanyi kodi tunakusanya. Tumezungumza mara kadhaa juu ya watanzania kuashiriki kwenye uchumi wa nchi yao kwa kupitia masoko ya mitaji katika soko la hisa DSE ili watanzania washiriki kwenye uchumi wao, tusiwanyime fursa wazawa kushiriki katika uchumi wao.”
Wakati Serikali ikiendelea kubanwa juu ya suala hilo, Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia amesema ukiligawanya deni hilo kwa idadi ya Watanzania milioni 45, kila mwananchi atakuwa anadaiwa Sh600,000.

Posted on 23:44 by Unknown

No comments

cesc-fabregas
Seke seke la usajili wa kiungo wa kimataifa wa Spain anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya La Liga limechukua hatua nyingine.
Fabregas ambaye anapiganiwa na vilabu vya Arsenal, Manchester United na Chelsea anatarajiwa kuuzwa baada ya kocha wake mpya Luis Enrique kuripotiwa kutokuwa na mpango nae kwenye utawala wake mpya Camp Nou.
Huku vita kubwa ikiwa inaendelea miongoni mwa vilabu vinavyomtaka, Katika mkutano wa waandishi wa habari wa timu ya taifa ya Spain inayojiandaa na michuano ya kombe la dunia, beki na mchezaji mwenzie Fabregas, Gerard Pique alisikika akimwambia kocha mkuu wa timu ya taifa ya Spain kwamba Cesc anaondoka Barcelona, na taarifa hizo ameambiwa na Fabregas mwenyewe.
Mazungumzo ya Pique na Del Bosque yalifanyika dakika chache kabla ya kuanza kwa mkutano, huku wakiwa hawajui kwamba vipokea sauti vimeawashwa wakawa wanazungumzia uhamisho wa Cesc.
Pique alisikika akisema: “Cesc Fabregas ameniambia uhamisho umekamilika, ameniambia amenunuliwa kwa Paundi milioni 33.”
Del Bosque akamjibu: “Maskini yule Rais (akimaanisha Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu). Hawezi kushinda namna.”

Posted on 23:41 by Unknown

No comments


TZA AFISA WA POLISI KENYA
Yule trafiki wakike wa Kenya ambae kwa sasa Wakenya wengi wanamuita Koplo Linda Okelo ameingia tena kwenye headlines huko huko Kenya na kwa sasa ameamua kwenda mahakamani kupinga hatua ya kamati ya kinidhamu iliyowekwa.
Hatua hiyo ni ya kuchunguza madai ya kuvaa sketi fupi ambayo imesemwa kuwa ilikua nje ya maadili ya kazi na sheria za Jeshi hilo la Polisi la nchini Kenya.
Kupitia kwa wakili wake Tom ojienda Koplo Lindah amesema kwamba hakufanya kosa lolote kuvaa sketi hiyo hadi kulazimika kuundwa kamati ya kumchunguza na kutoa maelekezo ya adhabu anayostahili.
Lindah amesema kwamba asubuhi ya April  26 alifanya mkutana na OCPD wa kituo cha kiambu ili kuelekezwa,ingawa mkuu huyo wa polisi hakusema lolote kuhusiana na mavazi aliyovaa.
Ingawa May 2 Lindah alichukuliwa hatua za kinidhamukwa kosa la kuvaa mavazi yaliyombana kulingana na sheria za huduma za polisi-alivyo kuwa amevalia sketi fupi iliyombana saa saba mchana nje ya tawi la benki ya KCB lililopo kiambu.
Linda amedai kwamba sketi iliyo zua utata alikabidhiwa na afisa anaye shughulika na sare za polisi mwaka 2003 na amekua akivaa kila siku na mabosi wake hawakuwahi kulalamika kabla ya tarehe 26 Aprili.
Wakili wake Ojienda amesema kwamba wakati wa kikao cha kamati hiyo may 7 na may 9 Bii Okelo alichukuliwa hatua kimakosa kwani hakukua na sababu za kumuhukumu kulingana na mavazi yake,kesi yake itatajwa june 12 mwaka huu.

Posted on 23:40 by Unknown

No comments

Siku chache baada ya taarifa za kutoka Morogoro zilizomhusu Mtoto Nasra ambaye kwa sasa ni marehemu ambaye alifungiwa kwenye box kwa miaka 4,leo kutoka idara ya Hekaheka za leo kuna taarifa za namna hiyo.
mtoto
Taarifa inasema kuwa kuna mwanamke alikuwa anaishi na msichana wake wa kazi amefanya unyama kwa msichana huyo kwa kumfungia ndani kwa miaka 3 na kumtesa kwa kumn’gata’kwa meno ikiwa ni pamoja na kumchoma na pasi.
Mengine amekua akimpiga kila sehemu ya mwili wa huyo binti huyo na kwa sasa ana makovu mpaka kwenye makalio na kitu ambacho hakijafamiaka ni msichana huyo kujisaifia haja ndogo kila baada ya dakika 5.

Posted on 23:38 by Unknown

No comments



 Chatu akiwa anatamba pembeni ya ukuta kuingia ndani ya nyumba
 
Chatu akiwa ndani ya eneo la hiyo nyumba
 
Hii imetokea Mkoani Arusha leo hii, Chatu mkubwa akiwa amefungwa kitambaa cheupe chenye maandishi ya kiarabu amekutwa kwenye nyumba ya mkazi mmoja wa Eneo la Sakina.
Majirani walipoanza kumvizia ili waweze kumuua walipata taarifa ya simu kutoka kwa Mwenye nyumba hiyo ambae ni tajiri mmoja wa huko Arusha akidai kuwa wasimuue huyo mtoto wake, lakini majirani hao hawakufata vile ambavyo huyo Mama alidai na hatimae walifanikiwa kumuua na kumkata kata vipande.
Baadhi ya watu wamehusisha kitendo hicho na imani ya kishirikina (Uchawi) hivyo kupelekea watu kuamini kuwa hata utajiri wake umetokana na mambo hayo.
 
 
  

Posted on 23:30 by Unknown

No comments



Hizi baadhi ya picha ambazo zimeenea kwenye mitandao ya jamii na zipo nyengine nyingi lakini kutokana na sababu za kimaadili si vema kuanika hapa maana ni aibu sana.
Lakini kwa mujibu wa Mh. John Komba amekanusha tukio hili na kusema kuwa Picha hizi ni za ku edit na kwamba si kweli kwamba yeye ni mchafu kiasi hicho.



Posted on 23:25 by Unknown

No comments