
Seke seke la usajili wa kiungo wa kimataifa
wa Spain anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya La Liga limechukua
hatua nyingine.
Fabregas ambaye anapiganiwa na vilabu vya
Arsenal, Manchester United na Chelsea anatarajiwa kuuzwa baada ya kocha
wake mpya Luis Enrique kuripotiwa kutokuwa na mpango nae kwenye utawala
wake mpya Camp Nou.
Huku vita kubwa ikiwa inaendelea miongoni mwa
vilabu vinavyomtaka, Katika mkutano wa waandishi wa habari wa timu ya
taifa ya Spain inayojiandaa na michuano ya kombe la dunia, beki na
mchezaji mwenzie Fabregas, Gerard Pique alisikika akimwambia kocha mkuu
wa timu ya taifa ya Spain kwamba Cesc anaondoka Barcelona, na taarifa
hizo ameambiwa na Fabregas mwenyewe.
Mazungumzo ya Pique na Del Bosque yalifanyika
dakika chache kabla ya kuanza kwa mkutano, huku wakiwa hawajui kwamba
vipokea sauti vimeawashwa wakawa wanazungumzia uhamisho wa Cesc.
Pique alisikika akisema: “Cesc Fabregas ameniambia uhamisho umekamilika, ameniambia amenunuliwa kwa Paundi milioni 33.”
Del Bosque akamjibu: “Maskini yule Rais (akimaanisha Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu). Hawezi kushinda namna.”
0 comments:
Chapisha Maoni