Chatu akiwa anatamba pembeni ya ukuta kuingia ndani ya nyumba
 
Chatu akiwa ndani ya eneo la hiyo nyumba
 
Hii imetokea Mkoani Arusha leo hii, Chatu mkubwa akiwa amefungwa kitambaa cheupe chenye maandishi ya kiarabu amekutwa kwenye nyumba ya mkazi mmoja wa Eneo la Sakina.
Majirani walipoanza kumvizia ili waweze kumuua walipata taarifa ya simu kutoka kwa Mwenye nyumba hiyo ambae ni tajiri mmoja wa huko Arusha akidai kuwa wasimuue huyo mtoto wake, lakini majirani hao hawakufata vile ambavyo huyo Mama alidai na hatimae walifanikiwa kumuua na kumkata kata vipande.
Baadhi ya watu wamehusisha kitendo hicho na imani ya kishirikina (Uchawi) hivyo kupelekea watu kuamini kuwa hata utajiri wake umetokana na mambo hayo.