Blogroll

Jumatatu





Mgeni rasmi Mkurugenzi msaidizi Wizara ya Sayansi na Teknolojia idara ya sayansi na ubunifu Dr. Magreth Komba akizindua kijarida cha WITTED kuashiri uzinduzi wa  mpango wa kuhamasisha wanawake kusomea uhandisi sayanzi na teknolojia.





Mgeni rasmi Mkurugenzi msaidizi Wizara ya Sayansi na Teknolojia idara ya sayansi na ubunifu  
Dr. Magreth Komba
 
 
 
 
 
Picha ya pamoja

Posted on 04:21 by Unknown

No comments


Azam FC mshambuliaji John Bocco katika hatua dhidi ya beki wa jiji la Mbeya.

Posted on 04:10 by Unknown

No comments


Kinshasa

Ufumbuzi riwaya imekuwa kupatikana kwa matatizo, ambayo ni pamoja na polisi kupokea rushwa, makosa ya usalama barabarani na masaa katika foleni .

Robots ni kushikamana na kompyuta kuu , na wamejenga katika kamera , ambayo ripoti ya makosa ya usalama barabarani katika muda halisi. Hii hupunguza hatari ya shughuli yoyote ya kukwepa, kama vile rushwa. Ukosefu wa binadamu hufanya kutekeleza sheria rahisi.Wao ni umbo kama polisi trafiki binadamu, na taa za barabarani nyuma yao na kifua .
Haja ya robots haya uliojitokeza kwa sababu madereva na watembea kwa miguu sawa walilalamika kuhusu shughuli ya kukwepa, na uvivu wa maafisa wa usalama barabarani.

Posted on 03:21 by Unknown

No comments

Jumamosi


Dressed to impress: England players (from left to right) Andros Townsend, Adam Lallana, Jermain Defoe, Leighton Baines, Steven Gerrard, Ashley Cole, Frank Lampard, Chris Smalling, Michael Carrick, Gary Cahill, John Ruddy and Rickie Lambert show off the Three Lions' Marks and Spencer suits for this summer's World Cup

Posted on 00:39 by Unknown

No comments


10254026_701605643237230_8580053565843709984_n_a1d9b.jpg
e_ea375.jpg10314714_701605389903922_6275387952947322384_n_f2661.jpg1959405_701582933239501_207281538074768844_n_36b4b.jpg10330495_701594153238379_6010293286524896578_n_56e1e.png1491721_701582799906181_6031344742742479472_n_c4220.jpg10169171_701577873240007_943124478303523100_n_4a945.png

Posted on 00:25 by Unknown

No comments





Tupo kwenye ukumbi AICC arusha kwenye kongamano la vyombo vya habari. Ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari

 

Posted on 00:23 by Unknown

No comments



DSC_0053
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.

“Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda.

Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.

“Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.

Posted on 00:20 by Unknown

No comments










Magari yaliyozama baada ya ardhi kumezwa na maji

 Wakati mvua kubwa zimenyesha Dar es salaam siku kadhaa zilizopita baadhi ya watu waliilalamikia Serikali kwamba imefanya uzembe manake kama ingekua imejenga miundombinu vizuri, maeneo ambayo yangekumbwa na maafuriko ni machache.
Post hii ni maalum kwa ajili ya hiki kilichotokea kwenye jiji la Baltimore Marekani ambapo mvua kubwa imesabisha kuzama kwa mtaa uliokua umejengwa vizuri kabisa lakini umemezwa na magari yaliyokua yamepaki juu yake.

 Screen Shot 2014-05-02 at 11.03.44 PM
Screen Shot 2014-05-02 at 11.04.01 PM

Posted on 00:14 by Unknown

No comments

http://4.bp.blogspot.com/-rup9GsnMX8U/U2HUdSljY_I/AAAAAAAARJQ/_LLk6yGItkM/s1600/02.jpg
Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwaasa wabunge wote kushiriki kikamilifu katika kamati zao kizalendo kwa kujali nchi yao ili ipatikane bajeti yenye tija kwa taifa leo (jana) wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.

http://2.bp.blogspot.com/-OtOFpq8RUKo/U2HUaITF4gI/AAAAAAAARJE/NyW2gFgsWlM/s1600/03.jpg 
Waziri wa Fedha Saada Mkuya  Salum akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya Serikali kwa wabunge leo (jana) jijini Dar es salaam inayotarajia kuanza kutumika kwa mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015.

http://3.bp.blogspot.com/-obOedfMxDaw/U2HUaSkfxvI/AAAAAAAARJA/KpjYbkiIICQ/s1600/04.jpgWaziri Mkuu wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda  akizungumza na wabunge wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam. 

Posted on 00:11 by Unknown

No comments

Ijumaa


Screen Shot 2014-05-02 at 1.26.42 PM
 Ni rasmi kwamba Clouds Media International imepewa leseni ya kurusha matangazo katika nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE) ambapo mkurugenzi Mtendaji Joseph Kusaga amesema sasa kituo cha Clouds TV kimataifa kitakuwa kikishuhudiwa na watu wa mataifa mbalimbali.
Clouds TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni maarufu sana kwa vijana nchini Tanzania, hata hivyo sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo kwenye Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa vipindi kwa watazamaji vitakavyorushwa kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa.
Akieleza zaidi Kusaga amesema “Leo ni siku ya kihistoria na alama ya hatua moja katika mpango wetu wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa kupitia matangazo kwa njia ya mitandao’’.

Screen Shot 2014-05-02 at 1.27.41 PM

Clouds TV kimataifa haitotoa tu burudani lakini pia itakuwa kiunganishi kwa waafrika waishio katika umoja wa nchi za falme za kiarabu pamoja na kuwapa fursa za kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina yao.
Vituo vya televisheni katika Umoja wa falme za kiarabu vipo vingi na vyenye ushindani mkubwa, lakini Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi ya kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika chaneli yenye uwezo wa kuwahudumia zaidi ya watazamaji takribani milioni 3.5 kutoka katika nchi za Afrika. Kwa sasa hakuna kituo kinachotoa huduma hii na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.
Clouds TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani, tamthilia, maigizo, ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za mashariki, magharibi na kusini mwa bara la afrika na itapatikana kwa watazamaji walio katika Umoja wa falme za kiarabu kupitia huduma ya IPTV inayotolewa na Etisalat na Du.
Clouds TV kimataifa itarushwa kupitia mamlaka ya Abu Dhabi ijulikanayo kama twofour54, ikiungana na vituo kama FOX na CNN.
Clouds TV kimataifa itaanza kurusha matangazo ya majaribio katika wiki chache zijazo kabla ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.

Posted on 07:36 by Unknown

No comments


Screen Shot 2014-04-30 at 2.08.18 AM
Mpaka sasa video hii imetazamwa zaidi ya mara laki moja na elfu 30 kwenye mtandao wa Youtube toka ianze kuonyeshwa April 29 2014 ikiwa ni video ya kipekee na ya kiwango kingine cha juu tofauti na ilivyozoeleka kwa Sauti Sol.
Mtandao wa Kenya ghafla.co.ke umeripoti kwamba imefahamika video hii imezuiwa kuchezwa kwenye TV stations mbalimbali za Kenya kwa sababu imevunja maadili.
Kwenye Mdundo Awards jana usiku Bien Aime wa Sauti Sol alisema mwanasheria wao anashughulikia ishu ya kufungiwa kwa video yao ambayo imeambiwa inachochea ngono kutokana na uwazi wa wanaookenana ndani yake.
Hii itakua video nyingine iliyochukua headlines zinazofanana na ile ya P Unit ‘you guy’ ambayo ilifungiwa na CITIZEN TV kwa sababu ya mrembo alieliachia umbo lake kwa sana.

Posted on 07:34 by Unknown

No comments



mlipuko
Usiku wa kuamkia leo Maafisa nchini Nigeria wametoa taarifa kuhusu mlipuko uliotokea na kuua watu 19 katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini 6 kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani pia magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya ambao uko karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.
 nyanya
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa,Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari,Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa.
Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja,Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao.

Posted on 07:32 by Unknown

No comments




Screen Shot 2014-05-02 at 3.03.24 AM

Home » General News » Kumbe hata Marekani kuna wanaohukumiwa kunyongwa kimakosa?


Kumbe hata Marekani kuna wanaohukumiwa kunyongwa kimakosa?

Screen Shot 2014-05-02 at 3.03.24 AM

Uchunguzi mpya uliofanywa nchini Marekani unaonyesha mmoja kati ya wafungwa 25 wa mauaji hakufanya kosa hilo hivyo zaidi ya asilimia 4 kati ya wafungwa wa kimarekani wamehukumiwa kifo lakini hawakutenda makosa hayo.
Wachunguzi kutoka Pennsylvania, Michigan na kwengineko wamekaa pamoja kuchunguza kitu kinachoitwa “Dark figure” yaani hesabu ya wafungwa waliohukumiwa kifo na wakati hawakufanya uhalifu unaowafanya wahukumiwe kifo.
Matokeo ya uchunguzi huo ambayo yalichapishwa na (National Academy of Science of the United States) yameonesha kuwa mauaji ya watu wasio na hatia yamekua kitu cha kawaida nchini humo.

Screen Shot 2014-05-02 at 3.10.17 AM

Walionyongwa/kuuliwa bila ya hatia wamezidi kutoka asilimia 1.6 mpaka asilimia 4.1 ambapo wafungwa 340 walikuwa wawe wameshatolewa ndani ya miaka 30 iliyopita na 138 kati yao walinusurika na adhabu hiyo.
Wengi walinusurika na adhabu hiyo kati ya miaka ya 1993 mpaka 2004 ambapo watu 2,675 walitolewa katika orodha ya kuuliwa baada ya uangalizi wa makini kufanyika tena katika kesi zao ambapo hiyo ni asilimia 36 ya watu waliokutwa na adhabu hii kati ya miaka hiyo.
Hata hivyo hawakuachiwa huru pamoja na kwamba waliondolewa adhabu ya kunyongwa  badala yake walipewa adhabu nyingine na wengi wao wakihukumiwa kifungo cha maisha.


Posted on 07:29 by Unknown

No comments



Kikosi cha United msimu uliopita.
Kikosi cha United msimu uliopita.
Wakati David Moyes alipoambiwa kuwa ameteuliwa rasmi kuwa kocha wa Manchester United baada ya Sir Alex Fergusson alikuwa na uhakika kuwa maisha yake kama kocha yatabadilika kwa kiasi fulani . Moja ya mazingira magumu aliyokuwa akikutana nayo akiwa Everton ni ufinyu wa bajeti ambayo ilikuwa inamfanya awe kwenye wakati mgumu kujaribu kupata wachezaji kwa bei za bure .
Moyes alidhani kuwa tatizo hilo linaweza kuwepo United na alishangaa alipoambiwa kuwa fedha si tatizo Man United tatizo ni yeye tu . Hiyo ndio kauli iliyotoka kwa wamiliki wa Manchester United ambao ni familia ya Glazer inayoongozwa na mzee Malcolm Glazer akisaidiwa na wanae Joe na Avram Glazer ambao wamesema kuwa wako tayari kumletea David Moyes Jembe lolote analotaka kulisajili ili mradi tu awe kwenye mazingira mazuri kwenye msimu wake wa kwanza.
David Moyes ambaye jana aliiongoza United katika mchezo wake wa kwanza ambao timu hiyo ilifungwa 1-0 na Thai All Stars amekuwa akiwasaka wachezaji kadhaa kimya kimya na kumekuwa na tetesi ambazo zimeihusisha United na wachezaji kama Gareth Bale , Cristiano Ronaldo na Thiago Alcantarra.
Hata hivyo hadi sasa United imepeleka ofa moja tu ya kumsajili beki wa kushoto Leighton Baines ya paundi milini 12 ambayo hata hivyo klabu ya Everton imeikataa. United wanaelekea kumkosa kiungo ambaye walitajwa kuwa mbioni kumsajili ambaye ni Thiago Alcantarra aliye karibu kukamilisha usajili kwenda Bayern Munich.

Posted on 07:23 by Unknown

No comments

Akon on kila muamerika mweusi arudi Afrika July 14 2013

Posted on 07:21 by Unknown

No comments




.

Naona hii ni historia kabisa aisee….. yani Rais Jakaya Kikwete anaweza hata kuingizwa kwenye kitabu cha kumbukumbu za dunia kwa kukubali mwaliko wa kuwa refa na kuchezesha mechi ya Wabunge wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wa timu za Simba na Yanga jumapili July 7 2013.
Taarifa ambayo nimepewa na Global Publishers ambao ndio waandaaji, ni kwamba Rais amekubali kuwa refa kwenye Tamasha la Matumaini litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambalo sehemu ya mapato yake yatasaidia elimu Tanzania.
Ni mara ngapi tunamuona President wetu kwenye sehemu rasmirasmi akiwa mgeni rasmi? ni mara ngapi tunatamani kuona upande wake wa pili kwenye ishu kama hizi? basi Jumapili hii itakua burudani na pia vichekesho… yani ukijaribu kutengeneza picha President na umri wake, na umbo lake, na cheo chake alafu apulize filimbi?????
Yani anakuwa refa na jezi zake kabisa…. na tumeshamzoea siku zote huwa anatokelezea hivi yani….


.
.
 

Posted on 07:20 by Unknown

No comments

NMB kwa kupitia idara yake ya biashara za Kilimo (Agribusiness Department) imetoa ripoti mbili;
1.Utafiti wa kujua kama mfumo wa stakabadhi mazao ghalani (Warehouse Receipt Financing Sytem) una manufaa kwa wakulima au la? Utafiti umethibitisha kuwa mfumo una manufaa kwa wakulima japokuwa kuna changamoto bado, mfano wakulima wa kahawa wanaouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wanapata zaidi ya asilimia 30% ukilinganisha na wale wasiotumia mfumo wa stakabadhi ghalani.
2.   Utafiti wa sekta ya sukari unaonesha kuwa Tanzania inatumia wastani wa tani 520,000 kwa mwaka (ikiwemo sukari kwa matumizi ya viwanda) kati ya hizo uzalishaji ni tani 300,000 na kiasi cha tani 220,000 zinaingizwa kutoka nje kwa mwaka,  utafiti pia umeonyesha kwamba Tanzania inaweza kuzalisha kiwango cha kutosheleza mahitaji ya nchi iwapo kutakuwa na kilimo cha umwagiliaji, miche bora ya miwa, pembejeo za kilimo zilizo bora ikiwemo mbolea pamoja na mazingira bora ya uwezeshaji (enabling environment) wa sekta ya sukari.
.
NMB wanaoshiriki maonesho ya Sabasaba yanayoendelea

. 
Maofisa wa NMB  Idara ya biashara ya Kilimo, kwanza kulia ni Sierk Plaat ambae ni  Mchambuzi Mwandamizi toka benki ya Rabobank, Robert Paschal Mkuu wa Idara Mikopo ya Kilimo NMB na Carol Nyangaro Mtafiti, Mchambuzi  wa mambo ya kilimo wakionyesha kitabu ambacho kimebeba ripoti ya mfumo wa stakabadhi  ghalani.




















































































































.
Mkuu wa Idara ya biashara za kilimo NMB, Robert Paschal (kati) akiongea na waandishi wa habari na kuwasilisha ripoti ya biashara za kilimo zifanywazo na Benki  ya NMB

Posted on 07:17 by Unknown

No comments