
Kikosi cha United msimu uliopita.
Wakati David Moyes alipoambiwa kuwa ameteuliwa rasmi kuwa kocha wa
Manchester United baada ya Sir Alex Fergusson alikuwa na uhakika kuwa
maisha yake kama kocha yatabadilika kwa kiasi fulani . Moja ya mazingira
magumu aliyokuwa akikutana nayo akiwa Everton ni ufinyu wa bajeti
ambayo ilikuwa inamfanya awe kwenye wakati mgumu kujaribu kupata
wachezaji kwa bei za bure .Moyes alidhani kuwa tatizo hilo linaweza kuwepo United na alishangaa alipoambiwa kuwa fedha si tatizo Man United tatizo ni yeye tu . Hiyo ndio kauli iliyotoka kwa wamiliki wa Manchester United ambao ni familia ya Glazer inayoongozwa na mzee Malcolm Glazer akisaidiwa na wanae Joe na Avram Glazer ambao wamesema kuwa wako tayari kumletea David Moyes Jembe lolote analotaka kulisajili ili mradi tu awe kwenye mazingira mazuri kwenye msimu wake wa kwanza.
David Moyes ambaye jana aliiongoza United katika mchezo wake wa kwanza ambao timu hiyo ilifungwa 1-0 na Thai All Stars amekuwa akiwasaka wachezaji kadhaa kimya kimya na kumekuwa na tetesi ambazo zimeihusisha United na wachezaji kama Gareth Bale , Cristiano Ronaldo na Thiago Alcantarra.
Hata hivyo hadi sasa United imepeleka ofa moja tu ya kumsajili beki wa kushoto Leighton Baines ya paundi milini 12 ambayo hata hivyo klabu ya Everton imeikataa. United wanaelekea kumkosa kiungo ambaye walitajwa kuwa mbioni kumsajili ambaye ni Thiago Alcantarra aliye karibu kukamilisha usajili kwenda Bayern Munich.
0 comments:
Chapisha Maoni