NMB kwa kupitia idara yake ya biashara za Kilimo (Agribusiness Department) imetoa ripoti mbili;
1.Utafiti
wa kujua kama mfumo wa stakabadhi mazao ghalani (Warehouse Receipt
Financing Sytem) una manufaa kwa wakulima au la? Utafiti umethibitisha
kuwa mfumo una manufaa kwa wakulima japokuwa kuna changamoto bado, mfano
wakulima wa kahawa wanaouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi
ghalani wanapata zaidi ya asilimia 30% ukilinganisha na wale wasiotumia
mfumo wa stakabadhi ghalani.
2. Utafiti
wa sekta ya sukari unaonesha kuwa Tanzania inatumia wastani wa tani
520,000 kwa mwaka (ikiwemo sukari kwa matumizi ya viwanda) kati ya hizo
uzalishaji ni tani 300,000 na kiasi cha tani 220,000 zinaingizwa kutoka
nje kwa mwaka, utafiti pia umeonyesha kwamba Tanzania inaweza kuzalisha
kiwango cha kutosheleza mahitaji ya nchi iwapo kutakuwa na kilimo cha
umwagiliaji, miche bora ya miwa, pembejeo za kilimo zilizo bora ikiwemo
mbolea pamoja na mazingira bora ya uwezeshaji (enabling environment) wa
sekta ya sukari.

NMB wanaoshiriki maonesho ya Sabasaba yanayoendelea

Maofisa
wa NMB Idara ya biashara ya Kilimo, kwanza kulia ni Sierk Plaat ambae
ni Mchambuzi Mwandamizi toka benki ya Rabobank, Robert Paschal Mkuu wa
Idara Mikopo ya Kilimo NMB na Carol Nyangaro Mtafiti, Mchambuzi wa
mambo ya kilimo wakionyesha kitabu ambacho kimebeba ripoti ya mfumo wa
stakabadhi ghalani.

Mkuu wa Idara ya biashara za kilimo NMB, Robert Paschal (kati) akiongea na waandishi wa habari na kuwasilisha ripoti ya biashara za kilimo zifanywazo na Benki ya NMB
0 comments:
Chapisha Maoni